People's Health Movement PHM - re-establish health and equitable development as top priorities with comprehensive primary health care


home page contact us     

About PHM News Room Events PHM Worldwide Campaigns Publications

Charters Voices PHA 2000 Links Get Involved Spanish
 Swahili

Last Update:  March 14, 2005 

 
Quick Feedback
Has this information been
useful? Yes    No
Name
Email
Keep me informed
Thank you

 
  Endorse the Charter

click here
to endorse the Charter

Endorse
Arabic
Bangla
Chinese
Danish
Dutch
English
Farsi
Filipino
Finnish
French
German
Greek
Guarani
Hausa
Hindi
Indonesian
Italian
Japanese
Kannada
Malayalam
Nepalese
Portuguese
Quichua
Russian
Sinhala
Spanish
Swahili
Swedish
Urdu

 

    Download the Charter
Instructions about downloadable versions of the People's Charter for Health are on the publications page.

 

 

Mkataba Wa Afya Ya Jamii

Mkataba Wa Afya Ya Jamii
 
Download the   doc  | This document in pdf formatpdf   version


Mwaka 1978 kwenye mkutano mkuu wa Alma – Ata, mawaziri kutoka nchi wanachama 134 wenye mahusiano na Shirika la Afya Duniani (WHO) na shirika la Kimataifa la Elimu la Kuhudumia Watoto (UNICEF) walitoa tamko la “Afya kwa Wote ifikapo mwaka 2000”, kwa kuchagua “Huduma ya msingi ya afya kwa Jamii” (PHC) kama chombo cha kusaidia kutimiza azma hii.

Bahati mbaya, ndoto hizi hazikutimizika. Hali ya afya ya watu katika dunia ya tatu haikuboreka. Katika namna mbali mbali imedhoofika zaidi. Hivi sasa tunapambana na tatizo la afya duniani, ikihusisha kuongezeka kwa tofauti ndani na baina ya nchi. Tishio jipya katika afya linaendelea kujitokeza. Matatizo haya yanakuwa magumu zaidi kutokana na msukumo hasi wa utandawazi ambao unazuia mgawanyo sawa wa rasilimali ukihusisha afya za watu na hasa afya za wale masikini.

Katika sekta ya afya, kushindwa kutekeleza mambo ya msingi ya afya ya msingi ya jamii, kama ilivyokusudiwa mwanzo katika Alma – Ata, kumeongeza kwa kiasi kikubwa tatizo la afya duniani. Serikali na mashirika ya kimataifa yanahusika kikamilifu katika kushindwa huku. 

Sasa imekuwa muhimu kuweka juhudi ya pamoja kimataifa ili kuweka malengo ya afya kwa wote katika hali inayofaa katika ajenda ya maendeleo. Kwa hakika uvumbuzi unaomlenga mwananchi hauna budi kuimarishwa ili kuongeza kwa watoa maamuzi, serikali na hata sekta binafsi ili kuhakikisha kwamba dira ya Alma - Ata inafikiwa. 

Baadhi ya Asasi za Kimataifa na Mashirika ya Jamii, Asasi zisizo za kiserikali na vikundi vya wanawake wameamua kufanya kazi pamoja kufikia lengo hili. Kundi hili kwa pamoja na mengine yenye kujitolea katika afya ya msingi na hali ya mtizamo wa watu, yaliandaa “Mkutano wa Afya ya Jamii” ambao ulifanyika toka tarehe 4 – 8 Desemba 2000 huko Bangladesh, Savar katika kituo cha Gonoshasthaya Kandra ama GK (kituo cha Afya ya Jamii).

Washiriki 1,453 kutoka nchi 92 walihudhuria mkutano huo ambao ulifikia upeo baada ya matayarisho ya miezi tisa 18 kote duniani. Mchakato wa matayarisho ulileta hamasa isiyo kifani na ushiriki wa watu wa aina mbali mbali ambao walijihusisha katika maelfu ya mikutano ya Vijiji, warsha katka ngazi za Wilaya na mikusanyiko ya kitaifa.

Vipindi vya majadiliano (plenary) vililenga mada kuu tano: Afya, Maisha na Hali njema; Kutokuwa sawa, Umasikini na Afya; Utunzaji wa Afya na Huduma za Afya; Mazingira na kuishi na mambo ya mbele.

Watu kutoka pande zote za dunia walitoa shuhuda za kunyimwa na kukosa huduma pamoja na shuhuda za uvumbuzi uliofanikiwa wa watu na mashirika. Zaidi ya vipindi mia vilivyoendeshwa wakati mmoja vilisaidia washiriki kubadilishana mawazo na kujadili kiundani mambo mbali mbali ya vipengele muhimu na kutoa sauti kwa ujuzi maalumu na mashaka yao.

Tukio la siku tano liliwawezesha washiriki kujieleza katika lugha zao na namna yao wenyewe. Waliweka bayana kushindwa kwa serikali zao na mashirika ya kimataifa na kuamua kupigana kwa pamoja ili afya na maendeleo yaliyosawa yapewe kipaumbele katika ajenda za watunga sera kuanzia ngazi za vijiji, taifa na kimataifa.

Katika kuchambua matatizo na shida zao na kubadilishana ujuzi wao, washiriki walitengeneza na kutia sahihi Mkataba wa Afya ya Jamii. Mkataba huu tangu sasa utakuwa ni chombo maalumu cha wote duniani, cha wananchi wenye ari na nia ya kutimiza ndoto za kukamilisha yaliyokuwa kwenye Alma–Ata. Tunatia moyo na kukaribisha yeyote mwenye kuwa na mashaka kama sisi na kuwa na kusudio kama letu watuunge mkono kwa kutia sahihi Mkataba huu. 


Mkataba Wa Afya Ya Jamii

Dibaji:
Afya ni jambo la kijamii, kiuchumi na kisiasa, na zaidi ya hayo msingi wa haki ya binadamu. Kutokuwepo usawa, umasikini, unyonyaji, mateso na udhalimu ni vyanzo vya afya mbaya na vifo vya watu masikini na wasio na uwezo. Afya kwa wote inamaanisha kupingana na dhamira zenye nguvu ya mamlaka, kupigana na utandawazi, na kuyapa kipaumbele mabadiliko ya kiuchumi na kisiasa.

Mkataba huu una uhusiano na sauti za wananchi ambazo awali hazikuweza kusikika kabisa. Inatia moyo watu kuweza kutafuta ufumbuzi wao wenyewe na kuwajibisha tawala zao za wananchi, serikali za mataifa yao, Asasi za kimataifa na ushirika.


DIRA.
Usawa na maendeleo endelevu kimazingira na amani ni kiini cha dira yetu ya kuwa na dunia nzuri – dunia ambayo afya kwa wote ni yenye uhakika, dunia ambayo inaheshimu, inathamini na kushangilia maisha yote na kwa namna mbali mbali; dunia inayowezesha kupanuka kwa vipaji na uwezo wa watu ili kustawishana, dunia ambayo sauti za wananchi zitaongoza maamuzi yatakayoelekeza maisha yetu. 

Kuna raslimali nyingi kupita kiasi kuwezesha kukamilisha azma ya dira hii. 


TATIZO LA AFYA.

“Magonjwa na vifo vya kila siku vinatukasirisha. Siyo kwa sababu kuna watu wanaugua ama kwa sababu kuna watu wanaokufa. Tumekasirika kwa sababu maradhi na vifo vingi kiini chake ni sera za kiuchumi na kisiasa tulizoletewa.
 

(sauti kutoka Amerika ya Kati) 



Katika miongo ya karibuni, mabadiliko ya kiuchumi duniani kote yameathiri sana afya za watu na upatikanaji wa tiba na huduma nyingine za jamii.

Licha ya utajiri usiokifani ulioko duniani, umasikini na njaa vinaongezeka. Tofauti kati ya mataifa tajiri na masikini inaongezeka; kama ilivyo kutokuwa na usawa miongoni mwa nchi na nchi, kati ya makundi ya kijamii, kati ya wanawake na wanaume na kati ya vijana na wazee.

Sehemu kubwa ya watu duniani bado upatikanaji wa chakula, elimu, maji safi na salama ya kunywa, mazingira safi, makazi, ardhi na raslimali zake, ajira na huduma za afya ni wa shida. Ubaguzi unaendelea kutawala. Unaathiri utokeaji wa magonjwa na uapatikanaji wa huduma ya afya. 

Raslimali za dunia zinamalizika katika kiwango cha kutisha. Uharibifu wa mazingira unatishia afya ya kila mtu, hasa afya ya watu masikini. Kumekuwa na kuibuka kwa Migogoro mipya wakati silaha za maangamizi zinatishia kwa kiwango kikubwa. 

Rasilimali za dunia zinazidi kuwa mikononi mwa wachache wanaokazana kupata faida binafsi maradufu. 
Mtizamo mpya wa kisiasa na sera za kiuchumi, zinawekwa na kundi dogo la serikali zenye nguvu, na mashirka ya kimataifa kama vile Benki ya Dunia (WB), Shirikaa la Fedha Duniani (IMF) na Shirika la Biashara la Dunia (WTO). Sera hizi pamoja na shughuli zisizo na mwelekeo za mashirika haya makubwa, zimechangia katika kudidimiza maisha ya watu na jinsi ya kupata riziki zao, afya na hali njema ya maisha kote, Kaskazini na Kusini. 

Huduma za jamii hazikidhi mahitaji ya watu hata kidogo, kwa sababu zimeathiriwa na kukatwa kwa bajeti za serikali zinazohusu huduma za jamii.
Huduma za afya zinapatikana kwa shida na hazisambazwi kwa uwiano na kwa usahihi.

Ubinafsishaji unatishia kudhoofisha upatikanaji wa huduma za afya zaidi na kuleta mashaka zaidi katika misingi ya usawa.

Kuendelea kuwepo kwa magonjwa yenye kinga, kuibuka tena kwa magonjwa kama kifua kikuu (TB) na malaria, na utokeaji na usambaaji wa magonjwa mapya kama VVU/UKIMWI (HIV/AIDS) ni kielelezo na kumbukumbu tosha ya jinsi dunia yetu isivyowajibika katika misingi ya haki na usawa. 


MISINGI YA MKATABA WA AFYA YA JAMII. 

  • Kufikiwa kwa kiwango cha juu cha afya na hali njema ni haki ya kibinadamu, bila kujali rangi ya mtu, kabila, dini, jinsia, umri, uwezo, maelekezo ya jinsi au tabaka.

  • Misingi ya pamoja yenye mambo mengi yahusuyo Huduma ya Afya ya Msingi (PHC), iliyoko kwenye Azimio la Alma – Ata la mwaka 1978, sharti iwe ndiyo msingi wa kutunga sera zinazohusiana na afya. Sasa, kuliko ilivyo kawaida, usawa, ushirikishwaji na ushirkiano wa kisekta kwa afya na huduma ya afya vinahitajika.

  • Serikali zina jukumu la msingi la kuhakikisha upatikanaji wa afya bora kwa wote, elimu na huduma nyingine za kijamii kulingana na matakwa ya watu na siyo kulingana na uwezo wao wa kulipa.

  • Kushiriki kwa watu na mashirika ya jamii ni muhimu katika uanzishaji, utekelezaji na utathmini sera zote na programu za afya na za kijamii.

  • Afya kimsingi inahusishwa na siasa, uchumi, jamii na mazingira halisi, na pamoja na usawa (equity) na maendeleo endelevu, haina budi iwe ni kipaumbele cha kwanza katika uundaji wa sera za jamii katika ngazi za chini, kitaifa na kimataifa.
     

WITO WA UTEKELEZAJI.

Katika kukabiliana na tatizo la afya ulimwenguni, tunahitaji kuchukua hatua katika ngazi zote - kibinafsi, kijamii, kitaifa, kikanda na kidunia na katika sekta zote. Matakwa yaliyoainishwa hapa chini ni kiini cha utekelezaji.


AFYA KAMA HAKI YA BINADAMU.

Afya ni mfano wa uwajibikaji wa jamii katika usawa na haki. Afya na haki za binadamu lazima ziendane na maswala ya uchumi na siasa.


MKATABA HUU UNATOA WITO KWA WATU WOTE DUNIANI.

  • Kutoa msaada katika hatua zote za utekelezaji wa haki ya afya.

  • Kutoa shinikizo kwa serikali na mashirika ya kimataifa kuunda upya, kutekeleza na kuwekea mkazo sera na utendaji unaotathmini haki ya afya.

  • Kujenga uwezo wa vikundi vya kutoa shinikizo kwa serikali kuingiza afya na haki za binadamu katika katiba na sheria za nchi.

  • Kupinga matumizi mabaya ya mahitaji ya afya ya jamii kwa matumizi ya kujipatia faida.
     

KUKABILIANA NA VIPENGELE VIKUU VINAVYOATHIRI AFYA.

Uchumi una msukumo mkubwa kwa afya ya jamii. Sera za kiuchumi zinazotoa kipaumbele kwa haki, afya na ustawi wa jamii zinaweza kuboresha afya ya watu na vile vile uchumi.

Sera za kisiasa, kiuchumi, kilimo na kiviwanda ambazo kimsingi zinaendana na matakwa ya kibepari, zilizowekwa na serikali za nchi na mashirika ya kimataifa, zinawatenga watu katika maisha yao na jinsi wanavyoendesha maisha. Mfumo wa uchumi wa utandawazi na mabadiliko, umeongeza tofauti kati na baina ya mataifa. Nchi nyingi duniani na hasa zenye uwezo zinatumia raslimali zake pamoja na vikwazo vya kiuchumi na kuingilia kijeshi, kuikusanya nguvu na kupanua wigo wao, ikiwa ni pamoja na kuleta athari kubwa kwa maisha ya watu.

Mkataba huu unatoa wito kwa watu ulimwenguni:

  • Kudai mabadiliko ya Shirika la Kibiashara la Kimataifa (WTO) na mfumo wa biashara duniani ili kupunguza ukiukaji wa haki za kijamii, kimazingira, kiuchumi na afya na kuanza kubadilika kwa kuzipa upendeleo nchi za Kusini ili kulinda afya ya jamii. Mabadiliko haya lazima yaendane na haki za ubunifu za mali (kama vile haki ya kukataza kuiga uvumbuzi – CHATAZA) na masuala yanayohusiana na biashara ya Haki za Ubunifu za Mali (Intellecture Property Rights agreement - “TRIPS”).

  • Kudai kufutwa kwa madeni ya nchi za dunia ya tatu.

  • Kudai mabadiliko ya haraka (radical) ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha duniani ili taasisi hizi ziendane na kuinua bayana haki na maslahi ya nchi zinazoendelea.

  • Kudai kanuni zinazofaa ili kuhakikisha kuwa TNCS hazina madhara kwa afya za watu, haziharibu nguvu kazi yao, hazichakazi mazingira ama kuathiri uhuru wa taifa.

  • Kuhakikisha kuwa serikali zinatekeleza sera za kiuchumi kuendana na matakwa ya watu na siyo kukidhi matakwa ya masoko, na hivyo kutoa uhakika wa chukula na haki ya kukipata chakula hicho.

  • Kudai kuwa serikali za kitaifa zilinde haki za afya kwa umma katika sheria ya haki ya ubunifu (intellectual property laws).

  • Kudai kudhibiti na kutoza ushuru wa mtiririko wa fedha wa kimataifa (speculative internatiaonal flows).

  • Kusisitiza kuwa sera zote za kiuchumi ziendane na afya, haki, jinsia na tathmini ya athari za kimazingira na kuhusisha hatua za marekebisho zinazotiliwa mkazo ili kuhakikisha panakuwepo makubaliano.

  • Kupingana na nadharia za ukuzaji uchumi badala yake iwekwe mibadala inayojenga ubinadamu na jamii yenye nguvu. Nadharia za kiuchumi lazima ziatambue matatizo ya kimazingira, umuhimu mkubwa wa haki na afya, na mchango unaofanywa na kazi zisizo na malipo, na hasa kazi zisizotambulika zinazofanywa na wanawake.
      

 
CHANGAMOTO ZA KIJAMII NA KISIASA.

Sera za kijamii zinazoeleweka zina matokeo mazuri kwa maisha ya watu na upataji wa riziki. Utandawazi wa kiuchumi na ubinafsishaji vimeleta athari kubwa kwa kusambaratisha jamii, familia na utamaduni. Wanawake wana umuhimu katika kuunganisha jamii katika kila sehemu. Lakini mahitaji yao ya msingi mara nyingi hayathaminiwi na hata kukataliwa, na haki zao na utu kutojaliwa.

Taasisi za kijamii zimedharauliwa na kudhoofishwa. Majukumu yake mengi yamehamishiwa sekta binafsi, hasa mashirika au kwenye taasisi zingine za kitaifa ama kimataifa, ambazo haziwajibiki kamwe kwa jamii. Zaidi ya hapo, uwezo wa vyama vya siasa na vya wafanyakazi umeathiriwa vibaya, wakati kutobadilika na msukumo wa imani kali kisiasa vinaongezeka. Demokrasia ya ushirikishwaji katika mashirika ya kisiasa na miundo ya kijamii (civic structures) ni lazima vidumishwe.
Kuna umuhimu mkubwa wa kuendeleza na kudumisha uwazi na uwajibikaji.

Mkataba huu unatoa wito kwa watu ulimwenguni:

  • Kudai na kusaidia maendeleo na utekelezaji wa sera za kijamii kwa kushirikisha watu kikamilifu.

  • Kuhakikisha kuwa watu wote wanawake kwa wanaume wana haki ya kufanya kazi, kutafuta riziki, kuwa na haki ya kujieleza, kushiriki kisiasa, kuabudu dini waitakayo, kupata elimu na kuwa na uhuru kutokana na matumizi ya nguvu.

  • Kushinikiza serikali kuanzisha na kutekeleza sheria za kulinda na kuboresha afya kimwili, kiakili na kiimani na haki za binadamu za makundi yaliyotengwa.

  • Kudai maswala ya elimu na afya yapewe kipaumbele katika ajenda za kisiasa. Hii inamaanisha kuwa na elimu ya bure na bora kwa watoto wote na watu wazima, na hasa watoto wa kike na wanawake, na hasa elimu na matunzo bora ya utotoni.

  • Kudai kuwa shughuli zote za taasisi za kijamii, kama vile huduma za matunzo ya watoto, mifumo ya ugawaji chakula, utoaji wa makazi, vinasaidia afya za mtu mmoja mmoja na jamii pia.

  • Kulaani na kutafuta mabadiliko ya sera ambazo zinasababisha ukosefu wa ardhi, makazi na kazi kwa jamii.

  • Kupinga siasa kali zinazotishia haki na uhuru wa mtu binafsi na hasa maisha ya wanawake, watoto na walio wachache.

  • Kupinga utalii na biashara ya kuuza miili na usafirishaji wa wanawake na watoto duniani.
     

CHANGAMOTO ZA KIMAZINGIRA.

Uchafuzi wa maji na hewa, mabadiliko ya ghafla ya hali ya hewa, kuliwa kwa hewa ya ozoni, nishati za nuklia na taka zake, kemikali zenye sumu na madawa ya wadudu, uharibifu wa bioanuai, ukataji wa misitu na mmomonyoko wa ardhi, vimeleta athari kubwa kwa afya za watu.

Chanzo kikuu cha uharibifu huu ni pamoja na matumizi yasiyoendelevu ya rasilimali, kutokuwepo na mtizamo wa muda mrefu, ukuaji wa ubinafsi na kujengeka kwa tamaa iliyokithiri ya kupata faida isiyokifani, na matumizi ya ziada ya matajiri. Uharibifu huu ni lazima ukabiliwe na ubadilishwe mara moja na kwa uhakika.

Mkataba huu unatoa wito kwa watu wote ulimwenguni:

  • Kuyawajibisha mashirika ya kitaifa na kimataifa, taasisi za kijamii na majeshi kwa uharibifu wao uliokithiri na shughuli zao za hatari zinazoathiri mazingira na afya za watu.

  • Kudai kuwa miradi yote ya maendeleo ifanyiwe tathmini kama inakidhi vigezo vya kiafya na mazingira na kwamba tahadhari zichukuliwe endapo teknolojia na sera zinahatarisha afya na mazingira kama hatua za tahadhari.

  • Kuomba serikali ziwajibike katika kupunguza gesi zinazochafua mazingira katika himaya zao zaidi kuliko kulenga iliyowekwa kwenye makubaliano ya mashirika ya hali ya hewa, bila kuingia kwenye uchafuzi au matumizi na ama teknolojia zisizo sahihi.

  • Kupinga uhamasishaji wa bidhaa zenye hatari na sumu na taka za mnururisho (radio active) kupelekwa katika nchi maskini na jamii duni na kuhamasihsa suluhisho ambalo linapunguza bidhaa za taka.

  • Kupunguza matumizi makubwa na mtindo wa maisha yasiyo endelevu – kote Kusini na Kaskazini. Kushinikiza mataifa tajiri kupunguza matumizi yao na uchafuzi kwa asilimia tisini (90%).

  • Kudai zichukuliwe hatua za kuhakikisha taaluma ya afya na usalama, pamoja na ufuatiliaji wa hali za kazi unaomlenga mfanyakazi.

  • Kudai zichukuliwe hatua za kupunguza ajali na majeruhi sehemu za kazi, ndani ya jamii na majumbani.

  • Kukataa uigaji wa uvumbuzi wa kimila wa ujuzi wa kale na maliasili.

  • Kutunga viashiria maendeleo ya kimazingira na kijamii vinavyowalenga wananchi na jumuiya na kuanzisha na kuhakiki hali halisi ya uharibifu wa mazingira na hali ya afya ya watu.
     

VITA, MACHAFUKO, MIGONGANO NA MAJANGA YA ASILI.

Vita, machafuko, migongano na majanga ya asili yanaharibu na kusambaratisha utu wa mwanadamu. Vina athari kubwa kwa hali na fikra za kiafya kwa jamii, hasa kwa wanawake na watoto. Kuzidi kujilimbikizia silaha na mapambano na uuzaji wa silaha kimataifa kwa magendo kunatishia kuimarika kijamii, kisiasa na kiuchumi na mgawanyo wa raslimali katika sekta ya jamii.

Mkataba huu unatoa wito kwa watu wa ulimwengu:

  • Kusaidia kampeni na mwenendo wa kutafuta amani na upunguzaji wa silaha. 

  • Kuunga mkono kampeni dhidi ya uchokozi, na utafiti, utengenezaji na majaribio na matumizi ya silaha kali za maangamizi na silaha nyingine, pamoja na aina zote za mabomu ya ardhini.

  • Kuunga mkono jitihada za wanachi kufikia haki na amani ya kudumu, na hasa kwenye nchi zenye vita vya wenyewe kwa wenyewe na mauaji ya maangamizi.

  • Kulaani matumizi ya watoto kama askari wa vita, kulawiti na kuwabaka, kutesa na kuua wanawake na watoto.

  • Kudai kutokaliwa kwa nchi kimabavu ikiwa ni moja ya mbinu haribifu ya utu wa binadamu.

  • Kupinga matumizi ya kijeshi katika utoaji misaada ya kibinadamu.

  • Kudai mabadiliko katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ili liweze kufanya kazi zake kidemokrasia.

  • Kudai Umoja wa Mataifa na mataifa binafsi kusimamisha aina zote za vikwazo vinavyotumika kama mbinu ya kimabavu ambayo inaweza kuathiri afya ya raia.

  • Kuhimiza juhudi binafsi zinazowalenga watu ili kutangaza maeneo ya ujirani, jumuiya na miji kama maeneo ya amani na kanda zisizotakiwa kuwa na silaha.

  • Kuunga mkono harakati na kampeni za kuzuia na kupunguza ugandamizaji na tabia ya vurugu hasa kwa wanaume, katika kuleta na kuendeleza amani.

  • Kuunga mokono harakati na kampeni za kuzuia majanga ya asili katika kupunguza sana maumivu ya binadamu.
     

SEKTA YA AFYA INAYOWALENGA WANANCHI.

Mkataba huu unatoa wito wa utoaji wa Afya ya Msingi inayoeleweka dunuiani, bila kujali uwezo wa watu kulipia. Huduma za afya lazima ziwe za kidemokrasia na zinazoendana na rasilimali za kutosha zinazoweza kufanikisha azma hii.

Mkataba unatoa wito kwa watu duniani:

  • Kupinga sera za kimataifa na kitaifa ambazo zinabinafsisha huduma za afya na kuzigeuza kuwa bidhaa za kibiashara.

  • Kuitaka serikali kuendeleza, kutoa fedha na huduma muhimu za afya ya msingi kama njia pekee muhimu ya kushughulikia matatizo ya afya na kupanga huduma za afya kwa umma ili kuhakikisha huduma huru na zinazopatikana kwa wote.

  • Kuzishinikiza serikali kufuata na kutekeleza sera za afya na madawa kitaifa.

  • Kudai serikali zipinge ubinafsishaji wa huduma za afya ya jamii na kuhakikisha taratibu zenye kuleta nafuu katika sekta binafsi za afya huduma za afya za kujitolea na za Asasi Zisizo za Kiserikali (ASIZE).

  • Kudai mabadiliko muhimu ndani ya Shirika la Afya Duniani (WHO) ili liweze kuwajibka kwa ushindani wa huduma za afya ambazo zitawanufaisha masikini, ikizuia kutowashirikisha watu, ikihakikisha kazi za pamoja za kisekta, ikishirikisha mashirika ya watu katika mkutano wa Afya wa Duni (WHA) na kuhakikisha uhuru wa kutofungwa na maslahi ya taifa fulani. 

  • Kuendeleza, kusaidia na kuhusika katika shughuli za kuhamasisha nguvu za watu na kutawala maamuzi yao ya afya katika ngazi zote, ikijumuisha haki za mgonjwa na matumizi yake.

  • Kusaidia, kutambua na kuendeleza mifumo ya matibabu za jadi na wanaohusika nayo na jinsi wanavyohusika na Huduma za Afya ya Msingi.

  • Kudai mabadiliko katika mafunzo ya watumishi wa afya ili waweze kuyaelewa matatizo na utendaji wake waelewe athari za masuala ya kidunia katika jumuia zao, na wanatiwa moyo kufanya kazi na kuheshimu jamii na mazingira yake.

  • Kurahisisha techolojia ya tiba na afya (ikijumuisha dawa) na kudai ziwe sehemu ya mahitaji ya afya ya wananchi. 

  • Kudai utafiti wa afya, pamoja na utafiti wa jeni (nasaba) na kuendeleza madawa na teknolojia ya uzalishaji, vifanywe kwa ushirikiano vikilenga mahitaji ya watu na asasi husika. Lazima ziwe kanuni za afya ya zinazolenga watu na zenye kuheshimu maadili ya kiulimwengu.

  • Kusaidia haki za uzazi za watu na maamuzi ya kijinsia na kupinga matumizi ya nguvu katika sera ya idadi ya watu na upangaji uzazi. Msaada huu unahusisha haki za njia nzuri na salama za kurekebisha uzazi (fertility regulation).
     

 
USHIRIKISHWAJI WA WATU KWA LENGO LA KUDUMISHA AFYA ULIMWENGUNI.

Vyama na mikakati imara ndiyo msingi mkuu wa mchakato mzima wa uwazi, uwajibikaji na demokrasia katika utoaji maamuzi. Ni muhimu kuhakikisha haki za binadamu zinazingatiwa kisiasa, kijamii, kiuchumi, na kiutamaduni. Wakati Serikari zikiwa na jukumu la msingi la kuhakikisha kuna usawa katika kuendeleza afya na haki za binadama, vyama vya mahusiana ya kijamii na vyombo vya habari vina majukumu muhimu ya kuhakikisha kwamba sera na matakwa ya watu yanazingatiwa katika uundaji wa sera na kufuatilia utekelezaji wake. 

Tamko hili linawahitaji watu ulimwenguni wafanye yafuatayo:

  • Kujenga na kuimarisha asasi zitakazosimamia uchambuzi na utekelezaji.

  • Kukuza, kusaidia na kujihusisha kikamilifu kuhakikisha jamii katika katika ngazi zote inahusishwa katika maamuziyanayohusu huduma kwa jamii.

  • Vyama vya msingi vya kijamii vinawakilishwa katika mijadala na mikutano ya afya katika ngazi zote kuanzia halmashauri, kitaifa na kimataifa 

  • Kusaidia juhudi za jumuia katika ushirikishwaji kidemokrasia, kwa kuwawezesha kuwa na mahusianao ya karibu na jamii zingime ulimwenguni.
     

MKUTANO WA AFYA NA MKATABA. 

Mjadala dhidi ya Mkutano wa Kimataifa wa Afya (PHA) umedumu kwa zaidi ya muongo mmoja. Mwaka 1998 vyama mbali mbali vilizindua mchakato wa PHA na kuandaa mkutano mkuu wa Kimataifa uliofanyika Bangladesh mwishoni mwa mwaka 2000. Shughuli mbali mbali zilifanyika kabla na baada ya mkutano wa Bangladesh ikiwemo uendeshaji wa warsha za kikanda, ukusanyaji wa maelezo mbali mbali ya watu kuhusu afya na uandikaji wa rasimu ya Mkataba wa Afya ya Jamii. 
Mkataba huu umetayarishwa kutokana na mawazo ya pamoja, dira ya kuwa na afya bora ulimwenguni na mwito wa kuleta mabadiliko. Ni chombo cha araghibishaji (advocacy) na mahali pa kuanzia katika kujenga mtandao na katika shughuli za afya ulimwenguni kote. 

 

Ungana Nasi – Pitisha Mkataba.
Tunakaribisha na kuwahimiza watu wote na asasi zote kujiunga katika utandawazi huu, na kusaidia kudumisha utekelezaji wa Mkataba huu wa Afya ya Jamii (People’s Charter for Health). 

Barua pepe ya Sekretarieti ni:secretariat@phmovement.org  na sochara@vsnl.com  zote zitatumika hadi Machi 2003 na baada ya hapo itatumika sochara@vsnl.com.tu 

Tovuti: www.phmovement.org 
Anuani ya zamani ya Sekretarieti: 
PHA Secretariat, Gonoshasthaya Kendra, Savar, Dhaka, 1344, Bangladesh.

Anuani mpya ya Sekretarieti:
Community Health Cell,
367 Srinivasa Nilaya,
Jakkasandra 1st Main,
1st Block, Koramangala,
Bangalore 560 034, India
 
Simu: 91 – 80 – 5531518/5525372
Faksi: 91 – 80 – 5525372
Barua pepe: sochara@vsnl.com 
Tovuti: http://www.phmovement.org  au http://www.sochara.com 

 


Masahihisho
Baada ya kupitishwa kwa Mkataba wa Afya ya Jamii (PCH) tarehe 08.12.2000, kikundi kilichoandaa muswada wa Mkataba huu kilitakiwa kuviangalia upya vipengele vya utekelezaji namba 1 na 2 katika changamoto za kiuchumi ambavyo vilionekana vinaweza kufasiriwa kuwa vinaunga mkono ibara za kijamii zilizopendekezwa na WTO, ambazo lwa dhati yake zinaimarisha WTO na ajenda zake za mabadiliko mamboleo. Kwa vile hiyo inapingana na matakwa ya PHA ya kuibadilisha WTO na mfumo mzima wa biashara ulimwenguni, aya hizo mbili zimeunganishwa na kufanyiwa marekebisho. 

Kipengele cha machafuko ya kivita na migogoro ya kisiasa, vimerekebishwa ili kujumuisha majanga ya tokanayo na nguvu za asili. Kipengele kipya namba 5 kimeongezwa ili kudai kukomeshwa kwa mkazi vile vile kipengele namba 7. Kwa sasa kipengele namba 8, kilifanyiwa marekebisho na kinasomeka kukomesha aina zote za “KUTENGWA”. Kipengele kipya namba 11 kiliongezwa kinachohusiana na majanga yatokanayo na nguu za asili. 


Mkataba wa Afya ya Jamii (PCH – People’s Charter for Health)

*Naafiki na kukubaliana na ujumbe wa Mkataba
*Niko tayari kuunga mkono harakati hizi.
*Nadhamiria kuwa mwanachama hai wa Harakati.

(*Unaweza kuchagua kauli zote 3)

 

 

Jina:_________________________________________________________________________________

Asasi:________________________________________________________________________________

Anwani:______________________________________________________________________________

_____________________________________________________________________________________

_____________________________________________________________________________________

Simu:_______________________________________

Faksi:___________________________________

Barua pepe:___________________________________________________________________________

Tarehe:_______________________________________________________________________________

Sahihi:_______________________________________________________________________________

 

Tafadhali baada ya kujaza tuma kwa: 
Dr. Ravi Narayan,
Community Health Cell
367 Srinivasa Nilaya, 
Jakkasandra 1st Main,
1st Block, Koramangala
Bangalore 560 034 - India
 
Simu: 91 – 80 – 5531518/5525372
Faksi: 91 – 80 - 5525372
Barua pepe: sochara@vsnl.com 
Tovuti: www.sochara.com  au www.phmovement.org 

 

 

Quick Feedback: Has this information been useful?

 

 

 
 Back Home Up Next [include/copyright.htm]